Chama cha Mpira wa Miguu cha Ujerumani (DBU) kimetuma maombi ya
Hati ya Uhamisho wa Kimataifa (ITC) kwa wachezaji wawili wa Tanzania ili
wajiunge na klabu mbili tofauti za nchini humo.
Maombi hayo yaliyotumwa kwa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania
(TFF) ni kwa ajili ya wachezaji Henry Claud Egito aliyezaliwa Desemba 31, 1984
jijini Dar es Salaam, na Dominic Johnson aliyezaliwa Agosti 14, 1991 jijini
Tanga.
Wachezaji hao wanaombewa ITC kama wachezaji wa ridhaa. Egito
anaombewa hati hiyo ili ajiunge na klabu ya FSV Lokomotive Dresden wakati
Johnson anatakiwa na klabu na TSV 1967 Schwabbruck.
0 COMMENTS:
Post a Comment