Kocha wa Lipuli ya Iringa, Shadrack Nsajigwa amesema
ana imani kikosi chake kitakaa vizuri.
Nsajigwa amesema ana imani kubwa kwa kuwa wamekuwa
wakifanya marekebisho kila wanapocheza mechi za kirafiki. Kikosi chake
kinashiriki Ligi Daraja la Kwanza Tanzania Bara.
“Kikubwa uongozi umetusaidia kupata mechi za
kirafiki ndiyo maana tukasafiri hadi Dar es Salaam.
LIPULI |
“Tumekuwa tukijifunza kila tunapocheza bila ya
kujali tumeshinda au kupoteza mchezo.
“Kikosi changu kina mchanganyiko wa wakongwe na damu
changa na mechi hizi zinatusaidia kukijenga,” alisema Nsajigwa aliyekuwa
nahodha wa Yanga na timu ya taifa, Taifa Stars.
Mechi ya mwisho ya kirafiki ya Lipuli ilikuwa jana
ilipocheza na Simba kwenye Uwanja wa Kinesi jijini Dar na kulala kwa mabao 2-0.
Baadhi ya wakongwe walio katika kikosi hicho ni
Godfrey Bonny aliyewahi kucheza Yanga pamoja na Nsajigwa.
0 COMMENTS:
Post a Comment