September 9, 2013





Kipa namba moja wa Simba, Abel Dhaira na beki wa timu hiyo, Joseph Owino, wanatarajiwa kurejea Dar es Salaam, leo Jumatatu wakitokea kwao Uganda walikokuwa na matatizo mbalimbali.

Dhaira alikwenda nchini Uganda kufuatilia kesi iliyokuwa ikimhusisha kununua kiwanja ambacho tayari kilishauzwa kwa mtu mwingine huku Owino akienda nchini humo kushughulikia matatizo ya kifamilia.


Ofisa Habari wa Simba, Ezekiel Kamwaga, amesema tayari wameshawasiliana na nyota hao na watawasili leo Jumatatu tayari kwa kujiunga na wenzao kambini kujiandaa na mchezo dhidi ya Mtibwa Sugar.

Mchezo huo utapigwa Jumamosi hii kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

“Nafikiri tayari wameshakamilisha ishu walizokwenda kufuatilia, kwa hiyo kesho Jumatatu (leo), watawasili na kujiunga kambini moja kwa moja na wenzao,” alisema Kamwaga.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic