Mwanadada Serena Williams ameonyesha I kiboko ya njia baada ya kushinda tano la tano la mchezo wa tenisi la US Open kwa kumshinda Victoria Azarenka.
Rais mstaafu wa Marekani, Bill Clinton alikuwa kati ya watazamaji walioshuhudia mchezo mkali na wa kusisimua wakati Serena akitwaa taji hilo.
Serena ambaye ni namba moja kwa ubora duniani alimshinda Victoria Azarenka kwa seti 7-5 6-7 6-1 na haikuwa kazi lahisi.
Kutokana na ushindi huo, Serena alilamba
kitita cha pauni milioni 2.3 ikiwa ni malipo ya ushindi na bonas tokea kwanza
kwa michuano hiyo iliyokuwa na msisimko mkubwa. Hiyo inamfanya Serena amewa
ampata jumla ya pauni milioni 32 kwa mataji yake yote aliyowahi kushinda.
Azarenka anashikilia nafasi ya pili kwa ubora duniani, alitoa upinzani mkali lakini Serena akaonyesha yuko fiti zaidi.
Azarenka anaaminika ndiye mchezaji mgumu zaidi kukata tamaa katika mchezo wa tenisi, lakini bado Serena akawa mgumu na mkali zaidi yake hadi alipokubali.
0 COMMENTS:
Post a Comment