Simba
imeendeleza ushindi katika mechi zake za kirafiki baada ya kuilipua Lipuli ya
Iringa kwa mabao 2-0.
Katika
mechi iliyochezwa kwenye Uwanja wa Kinesi jijini Dar es Salaam, leo, Simba
ilipata mabao yake yote mawili katika kipindi cha kwanza.
Mabao
ya Simba yalifungwa na chipukizi wake Rashid Ismail Mkoko katika dakika ya 24
kabla ya Marcel Kaheza kufunga la pili katika dakika ya 28.
Lipuli
inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza inanolewa na beki wa zamani wa Yanga,
Shadrack Nsajigwa.
Pamoja
na kuwa daraja la chini lakini Lipuli ilionyesha soka la ushindani na kutoa
upinzani mkubwa kwa Simba.
Nsajigwa
alisema wataendelea kucheza mechi kadhaa za kirafiki kwa lengo la kuandaa
kikosi chao.
0 COMMENTS:
Post a Comment