September 30, 2013




Na Sophia Mwaipyana, Mbeya
 Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi, juzi aliwaacha hoi viongozi wenzake waliokuwa ndani ya Uwanja wa Sokoine jijini hapa, baada ya kupandisha mizuka.


Ilikuwa ni katika mchezo wa Ligi Kuu Bara kati ya Mbeya City na Coastal Union uliomalizika kwa sare ya 1-1.

Sugu, baada ya kuingia uwanjani hapo akiwa ndani ya gari lake, mashabiki walianza kumshangilia, kuona hivyo alishuka na kukimbia kuelekea jukwaani, kisha akakaa nao.

Akiwa jukwaani, Sugu alionekana kufurahia na kurukaruka kila Mbeya City ilipofanya vizuri na mashabiki walionekana kumfurahia na kuanza kumwimbia; ‘Sugu, sugu, sugu, sugu, sugu.’

Sugu alionekana kuwa tofauti kwani alikaa kwenye jukwaa la mashabiki, badala ya jukwaa kuu ambalo hutumiwa na viongozi. Muda wote alionekana kuwa na shangwe tele.

Baada ya mchezo huo, Sugu alitoka uwanjani kimyakimya na kutimka zake.
 SOURCE: CHAMPIONI

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic