September 11, 2013





Siku chache beki wa Yanga, Mbuyu Twite, kuingiliwa na wezi nyumbani kwake usiku wa manane na kumuibia baadhi ya vitu vyake vya ndani, juzi amekumbwa na hali mbaya tena baada ya kuibiwa simu.

Kipa huyo amesema aliibiwa simu yake aina ya Samsung yenye thamani ya shilingi shilingi 800,000.


Beki huyo ambaye alikuwa kama vile amechanganyikiwa alishindwa kulizungumzia jambo hili na kusema kuwa rafiki yake waliyekuwa naye aitwaye Eric ndiyo azungumze na waandishi.

Rafiki huyo anasema waliibiwa siku hiyo baada ya kusahua kufunga mlango wa gari wakati wakiweka mafuta kwenye kituo kimoja kilichopo Kinondoni.

 “Mbuyu alikuwa ndani ya gari anaongea na mweka mafuta nje na mimi nilikuwa nje kuna mtu naongea naye kwa hiyo wote tukawa bize, baada ya kuweka mafuta hatukuiona simu wakati ilikuwa imekaa sehemu nyeupe kabisa.

“Tukajaribu kuiangalia pale tukaikosa basi tukaondoka zetu lakini Mbuyu alisikitika sana, hata hivyo tumeshapeleka taarifa polisi kwa matukio yote hayo, wamesema tuwaachie wao wafanye uchunguzi kwanza” alisema rafiki wa mchezaji huyo aitwaye Eric

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic