Beki wa zamani wa Simba, Victor Costa,
amesema amepata timu tena nchini Msumbiji.
Kabla ya kurejea na kujiunga na Simba
tena, alikuwa nchini humo akiichezea timu ya Agasabe Disongo ya Jimbo la Tete.
Costa alisema amemalizana na Simba
vizuri na tayari amepata ofa ofa kutoka katika timu yake ya zamani pamoja na Ferraviaro
ya Beira.
“Nataka
kurudi na kuendelea kucheza soka nchini Msumbiji,” alisema Costa, mmoja wa
mabeki wakongwe nchini.
“Siwezi
kusema soka la hapa nchini baya ila limejaa ubabaishaji mwingi uliopitiliza
ukiangalia mchezaji awapo uwanjani anavyocheza kwa presha kwa kuhofia kuharibu
ili kulinda namba yake.
“Ndani ya mwezi mmoja suala langu
litakuwa limekamilika baada ya hapo nitapanga mipango yangu ya safari ya
kurejea Msumbiji nina imani Mungu yupo pamoja nami nitaangalia nikifika kule
timu itakayotoa ofa nzuri nitaingia mkataba nayo,”alisema Costa.
0 COMMENTS:
Post a Comment