Yule mwamuzi
aliyekutana na kipigo kutoka kwa wachezaji wa Yanga huku beki Stephano Mwasyika
akimchapa konde kali, ndiye atakayechezesha mechi ya watani Jumapili.
Israel Nkongo amepewa kazi ya kuamua mechi
hiyo yenye presha kubwa itakayopigwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar,
Jumapili.
Tafrani lilianza baada ya Nkongo kumlamba
Haruna Niyonzima kadi nyekundu ya pili na kumtoa nje.
Kutokana na kumpiga Nkongo, Simba walikuwa
wakiwatania Yanga kuwa ni mabondia na kila walipopoteza mchezo, basi waliimba
kuashiria hawajui mpira na badala yake ni ugomvi.
Mwamuzi huyo ambaye kitaaluma ni mwalimu,
wakati alilazimika kujichimbia na baadhi ya mashabiki wa Yanga walikuwa wakimpa
vitisho.
Lakini baadaye aliendelea na shughuli zake
kama kawaida akionekana kusahau katika mechi dhidi ya Azam FC ambayo Yanga
ililala kwa mabao 3-1.
0 COMMENTS:
Post a Comment