Iker Casillas atarejea leo kukichezea kikosi cha Real Madrid kitakapoivaa Copenhagen katika mechi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Kipa huyo aliumia katika mechi ya mwisho waliyocheza ya Ligi ya mabingwa na mwenyewe amesema kujiamini kwake ndiyo dawa.
"Vizuri kujiamini mwenyewe, matukio yanayotokea ni maisha ya kawaida ya kila siku. Hivyo ninachofanya ninaamini kiko sahihi.
“Yanayotokea sasa ni kipindi fulani ambacho hakifanani na kingine na maisha hayawezi kufanana kila siku,” alisema.
Casillas alisema hayo akionyesha kuwajibu wale ambao wamekuwa na hofu na mwishow ake hasa baada ya kuwa anapata nafasi kwa kugombea namba na kipa Diego Lopez aliyekuwa namba mbili kabla ya aliyekuwa kocha wa Real Madrid, Jose Mourinho kubadili mambo.
0 COMMENTS:
Post a Comment