Wakati
mabingwa wa soka Tanzania, Yanga wameamua kuhamishia mazoezi katika gym,
Mwenyekiti wao, Yusuf Manji leo aliungana nao ghafla na kufuatilia kwa karibu
kila kilichokuwa kinaendelea.
Katika
mazoezi hayo yaliyofanyika kwenye Gym maarufu ya Rio iliyo katika jengo la
Quality Centre jijini Dar, wachezaji hao walikuwa wakiendelea na mazoezi chini
ya benchi la ufundi linaloongozwa na Ernie Brandts.
Baada
ya kuingia katika Gym ya Rio, Manji alisimama mlangoni pamoja na daktari wa
timu, Nassor Matuzya na kuendelea kufuatilia kwa karibu kila kilichokuwa
kinaendelea.
Yanga
ilikuwa katika programu ya Gym na kesho itaendelea na mazoezi kama kawaida
kwenye Uwanja wa Shule ya Sekondari ya Loyola.
Yanga
itarudi tena uwanjani Jumapili kuwavaa Mtibwa Sugar ambao watakuwa wageni wao
kwenye dimba la Taifa.
0 COMMENTS:
Post a Comment