SIMBA VS JKT RUVU |
Mechi za Yanga na Simba za Ligi Kuu
ya Vodacom (VPL) zilizochezwa wikiendi iliyopita jijini Dar es Salaam
zimeingiza jumla ya sh. 182,103,000.
Yanga katika mechi yake dhidi ya
Ruvu Shooting iliyochezwa Jumamosi (Septemba 28 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar
es Salaam na kuibuka na ushindi wa bao 1-0 imeingiza sh. 94,202,000.
Watazamaji 16,492 walikata tiketi
kushuhudia pambano hilo ambapo kila klabu ilipata mgawo wa sh. 22,630,921.58.
Viingilio katika mechi hiyo vilikuwa sh. 5,000, sh. 8,000, sh. 15,000 na sh.
20,000, na Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) iliyolipwa ni sh. 14,369,796.61.
Mgawo mwingine wa mapato hayo ni
asilimia 15 ya uwanja sh. 11,507,248.26, tiketi sh. 3,117,215, gharama za mechi
sh. 6,904,348.96, Kamati ya Ligi sh. 6,904,348.96, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira
wa Miguu (FDF) sh. 3,452,174.48 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es
Salaam (DRFA) sh. 2,685,024.59.
Nayo Simba ambayo iliibuka na
ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya JKT Ruvu katika mechi iliyochezwa Jumapili
(Septemba 29 mwaka huu) katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam imeingiza sh.
87,901,000.
Watazamaji waliokata tiketi
kushuhudia pambano hilo namba 41 walikuwa 15,780. Viingilio katika mechi hiyo vilikuwa sh. 5,000, sh. 8,000, sh.
15,000 na sh. 20,000 huku kila klabu ikipata mgawo wa sh. 21,051,025.92 wakati
Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) iliyolipwa ni sh. 13,408,627.12.
Mgawo mwingine wa mapato hayo ni
asilimia 15 ya uwanja sh. 10,703,911.48, tiketi sh. 3,132,963, gharama za mechi
sh. 6,422,346.89, Kamati ya Ligi sh. 6,422,346.89, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira
wa Miguu (FDF) sh. 3,211,173.44, Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam
(DRFA) sh. 1,248,789.67 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Pwani (COREFA) sh.
1,248,789.67.
Wakati huo
huo, mechi ya
ligi hiyo kati ya Mbeya City na Coastal Union iliyochezwa Jumamosi
(Septemba 28 mwaka huu) Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya imeingiza
sh. 16,959,000 huku kila klabu ikipata sh. 4,035,229.
0 COMMENTS:
Post a Comment