October 14, 2013



Mabeki wa kati wa Yanga, Kelvin Yondani na Nadir Haroub ‘Cannavaro’ wote kwa pamoja wanamtaka kumkaba mshambuliaji wa Simba, Amiss Tambwe.                                                                                         


Tambwe mwenye mabao nane katika msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara hivi karibuni alitamba kuwa hakuna beki anayemhofia na kumuogopa Yanga kutokana na umahili wake mkubwa wa kupachika mabao.

Cannavaro amesema mshambuliaji huyo hana uwezo wa kumpita na kuisumbua safu yao ya ulinzi kutokana na viwango vyao vikubwa walivyokuwa ndani ya uwanja.

Cannavaro alisema, hatahakikisha mshambuliaji hapati bao katika mechi hiyo na hatapiga shuti katika goli kwa ajili ya kupunguza kasi yake ya kufunga mabao.

”Nimesikia sifa na jinsi anavyojitamba huyo Tambwe, sijui uwezo wake lakini namtamani sana nimkabe kwenye mechi ijayo tutakayocheza nayo.
“Nakwambiaje huyo mshambuliaji hatapata nafasi ya kupiga shuti golini kwetu na hata kufunga kwenye hasahau kutokana na ubora wa safu yetu ya ulinzi,” alisma Cannavaro.

Kwa upande wa Yondani alisema “Sijui uwezo wa mshambuliaji huyo, lakini kikubwa naomba Kocha wangu Mkuu, Ernest Brandts anipe jukumu la kumkaba huyo Tambwe.

“Kwanza huyo Tambwe mwenyewe ana uwezo gani wa kuogopwa, tusubilie tumuone siku huyo kama ataweza kufunga bao golini kwao” alisema Yondani.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic