October 7, 2013





Baada ya kuibeba Man United kwa kufunga mabao mawili muhimu, dogo, Adnan Januzaj anatarajia kuanza kulamba mshahara wa pauni 60,000 kwa wiki.


Januzaj ndiyo ana miaka 18 na mshahara huo tayari umekuwa gumzo kwa Mbelgiji huo.

Katika mechi hiyo aliyofunga mabao mawili dhidi ya Sunderland, imekuwa rekodi kwa kuwa ndiyo mechi yake ya kwanza kuanza katika Ligi Kuu England.

Tayari kinda huyo ni gumzo lakini mjadala umekuwa kama ni sahihi kuanza kupokea fedha hizo lukuki kwa umri alionao.
Lakini ubora wake unawalazimisha Man United kutoa ofa hiyo nono na mwisho mambo yanabaki vilevile, “kila mmoja atakula kwa urefu wa kamba yake.”

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic