October 7, 2013


TAMBWE AKIWA NA SALEH ALLY SIKU ALIPOWASILI NCHINI KWA MARA YA KWANZA

Na Mwandishi Wetu
MSHAMBULIAJI nyota wa Simba, Amissi Tambwe amesema yeye ni Mkristo safi tofauti na wengi wanavyofikiri.
 
Tambwe alizua gumzo baada ya kufunga bao lake la nane katika mechi dhidi ya Ruvu Shooting, juzi kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam na kuonyesha ishara ya msalaba.

Raia huyo wa Burundi alionyesha ishara hiyo mara tu baada ya kufunga bao hilo la mkwaju wa penalti baada ya mlinzi George Michael kumsukuma kwa makusudi Betram Mwombeki.

“Watu wengi sana leo wameniuliza swali hilo, waliniona nikionyesha ishara ya msalaba baada ya kufunga. Ukweli mimi ni Mkristo safi tokea kuzaliwa kwangu,” alisema na alipoulizwa kuhusiana na jina lake la Amissi, alisema:

“Ni jina la ukoo, nilipewa nikiwa mtoto. Lakini mimi ni Mkristo na sina jina tofauti na hilo. Suala hili limekuwa likiwatatiza wengi.”

Mrundi huyo tayari ana mabao manane na ndiye anaongoza kwa upachikaji wa mabao akifuatiwa na Themi Felix wa Kagera na Didier Kavumbagu wa Yanga wenye manane kila mmoja.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic