October 21, 2013

KAVUMBAGU (KULIA) AKIWA NA NIYONZIMA KUSHOTO. KIIZA (KATIKATI)

Kocha Msaidizi wa Simba, Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ amewavaa wachezaji wawili wa kimataifa wa Yanga na kusema anawashangaa kuporomosha matusi kwenye benchi la Simba.


Julio amesema kiungo Haruna Niyonzima, raia wa Rwanda na Didier Kavumbagu kutoka Burundi waliwatukana wachezaji na makocha waliokuwa kwenye benchi wakati wa mechi yao iliyomalizika kwa sare ya mabao 3-3, jana kwenye Uwanja wa Taifa, Dar.

“Nilishangazwa sana na wachezaji hawa, wao ni professional, tunategemea watakuwa na vitu tofauti. Lakini wanakuja na kutukana matusi ya nguoni.

“Imenishangaza sana, nakumbuka wlaipotufunga mbili bila walifanya hivyo. Sasa wamerudia na kutukana tena, tumewaangalia tu kwa kuwa sisi ni waungwana,” alisema Julio.

Alisema wachezaji hao walikwenda kwenye  benchi la Simba na kutukana matusi mara baada ya kuifunga Simba mabao matatu katika kipindi cha kwanza.
Salehjembe linawatafuta wachezaji hao wawili ili kujibu tuhuma hizo za Julio baada ya kujaribu kuwapata bila ya mafanikio.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic