Kikosi cha Simba kimetua mjini Tanga
huku viungo Haruna Chanongo na Abdulhalim Humud wakiachwa jijini Dar.
Sasa imebainika kwamba Humud na Chanongo
ndiyo wanaotuhumiwa kushindwa kucheza katika mechi dhidi ya Yanga ambayo Simba
ilisawazisha mabao matatu baada ya Kocha Abdallah Kibadeni kuwatoa.
Ingawa Kibadeni hakutaka kuwataja,
lakini aliangusha tuhuma kwamba kuna wachezaji wanaihujumu timu hiyo.
“Simba imefika Tanga kwa ajili ya mechi
ya Coastal Jumatano, lakini Chanongo na Humud wameachwa jijini Dar na
wametakiwa kuanza mazoezi na Simba B,” kilieleza chanzo.
Kuhusu hilo, Kibadeni alisema: “Nitawataja
tu, nitafute ila nikuhakikishie kuna tatizo.
“Niliwaambia kuwa kama wametaka kuipa
Yanga mabao, basi hizo tatu zinatosha na wanafanya makusudi kutofanya kazi.”
0 COMMENTS:
Post a Comment