Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), limetangaza si ruhusa kuingia uwanjani na silaha kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar.
Gazeti namba moja la michezo nchini la Championi, lilituma makachero wake ambao waliingia uwanjani hapo na silaha huku uongozi wa uwanja huo ukisisitiza kwamba ulinzi ulikuwa mkali.
Baada ya kuona hivyo, TFF na Jeshi la Polisi umetangaza hivi; kuanzia sasa halitashikilia silaha za washabiki, na badala yake
litawazuia kabisa kuingia viwanjani wakati wa mechi.
Jeshi la Polisi limekuwa likihifadhi silaha za washabiki
wanaokwenda viwanjani, na baadaye kuwarejeshea baada ya mechi kumalizika kwa
vile Kanuni za Usalama Viwanjani za Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu
(FIFA) zinakataza silaha viwanjani.
Wikiendi iliyopita katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, Jeshi la
Polisi lilikamata bastola 17 katika upekuzi wa washabiki waliokwenda kushuhudia
mechi kati ya Yanga na Ruvu Shooting na ile kati ya JKT Ruvu na Simba. Wote
waliokutwa na silaha hizo walikuwa na leseni za kuzimiliki.
Hivyo, kwa washabiki wanaomiliki silaha hatawaruhusiwa kabisa
kuingia viwanjani, na badala yake tunawashauri kuzihifadhi huko wanakotoka
kabla ya kufika viwanjani.
Pia tunatoa mwito kwa shabiki ambaye atamuona mwenzake akiwa na
silaha uwanja kutoa taarifa kwa mamlaka husika likiwemo Jeshi la Polisi ili
aweze kuchukuliwa hatua.
0 COMMENTS:
Post a Comment