SIKU AZAM TV WALIPOINGIA MKATABA NA TFF NA BODI YA LIGI KUONYESHA LIGI KUU YA VODACOM.. |
Azam Media Limited imefanikiwa kukamilisha utaratibu wa ushirikiano na Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) utakaowawezesha mashabiki wa soka kote nchini kunufaika kwa kuona michezo ya Ligi Kuu ya Vodacom.
Mechi za kila mwishoni mwa juma zitakuwa zikionekana katika TBC1 hadi kukamilika kwa nusu ya msimu wa 2013/14. Mechi hizo zitaonyeshwa kwa ya AzamTV.
Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) na Bodi ya Ligi (Kamati
ya Ligi) wameeleza kuunga mkono utaratibu huu makini.
“Baada ya kupata haki za matangazo ya luninga ya Ligi Kuu
ya Vodacom, moja ya shabaha zetu kuu imekuwa ni kuhakikisha kuwa tunafanikiwa
kurusha matangazo yanayokidhi viwango vya kimataifa kwa ubora.
“Ili kufanikisha shabaha hiyo tumewekeza vilivyo katika teknolojia
ya kisasa ya vifaa vya matangazo ya nje (Outside Broadcasting) na katika
mafunzo kwa watumiaji wa vifaa hivyo.
Ninayo furaha kusema kuwa matayarisho yamekwenda vema
kiasi kwamba tumejikuta tuko tayari kurusha matangazo ya kiwango cha juu kabla
hata ya kuzinduliwa kwa huduma kamili za AzamTV”, alisema Rhys Torrington,Ofisa
Mtendaji Mkuu wa Azam Media Limited.
“Kwa kuwa mashabiki wengi kote nchini wanangojea kwa hamu
kubwa kuziona timu wazipendazo, imeonekana ni vema kuanza kuonesha michezo hii
ya ligi sasa.
Kwa kuzingatia hali hiyo, nilifanya mazungumzo na rafiki
zetu pale TBC na kuwaomba iwapo wana uwezo na kuridhia kurusha matangazo
yetu ya moja kwa moja bila ya malipo yoyote kuanzia mwisho wa juma hili hadi
kukamilika kwa nusu msimu.
“ Tulifanikiwa kufikia makubaliano kwa haraka na sasa
tunafanyia kazi masuala ya kiufundi yatakayowezesha kuwa tayari kwa ajili ya
mchezo wa Jumamosi utakaofanyika Uwanja wa Taifa”, Aliongeza Torrington.
Mara tu huduma kamili za AzamTV zitakapozinduliwa majuma machache
yajayo, matangazo ya michezo ya Ligi Kuu kwa wigo mpana yatakuwepo pia kwenye
chaneli yake hadi mapumziko ya nusu msimu.
Baada ya hapo matangazo ya Ligi Kuu ya Vodacom
yatapatikana kwa wale tu watakaokuwa na visimbuzi (decorders) vya AzamTV.
0 COMMENTS:
Post a Comment