October 11, 2013





Kocha Mkuu wa Tanzania Prisons, Jumanne Chale amesema kuwa kipigo walichokipata Mgambo JKT basi watarajie kukipata wapinzani wao, Simba katika mechi ya Ligi Kuu kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, kesho.

Prisons itashuka dimbani ikiwa ni baada ya kupata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Mgambo Shooting, wkaati Simba pia ilipata sare ya bao 1-1- dhidi ya Ruvu Shooting.


Kocha huyo amesema kuwa maandalizi waliyoyafanya yanatosha kuwapa kipigo wapinzani wao mara watakapovaana.


“Nilichowafanya Mgambo Shooting kwenye mechi ya mwisho, ndiyo nitakachowafanyia Simba katika mechi hiyo, Simba hatuwaogopi lakini tunawaheshimu,” Chale ambaye timu yake inashika nafasi ya 11 ikiwa na pointi saba wakati Simba inaongoza ligi ikiwa na pointi 15.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic