October 11, 2013



 
NSAJIGWA ALIPOKUWA LIPULI
Uongozi wa Klabu ya Lipuli inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza umesema kuwa utapeleka barua ya kumshtaki kiungo wao, Geofrey Bonny na Shadrack Nsajigwa ambao wanaripotiwa kutoroka katika kikosi chao.


Geofrey alijiunga na Lipuli msimu huu ambapo alisaini mkataba wa mwaka mmoja na mpaka sasa ameitumikia kwa miezi miwili tu huku Nsajigwa akisaini miezi minne.
 
Mwenyekiti wa Lipuli Abuu Changawa amesema wapo kwenye mchakato wa kuiandaa barua hiyo kwa ajili ya kuipeleka na kudai haki yao kwa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).

Alisema nyota hao wa zamani wa Yanga waliondoka klabuni hapo bila kuaga huku wakitambua kuwa kila mmoja alikuwa amebakiza mkataba, kwa upande wa Bonny mpaka sasa amebakiza miezi 10 huku Shadrack Nsajigwa akiwa na miezi miwili kati ya minne aliyosaini kuifundisha timu hiyo.

“Hapa tunaandaa barua na muda wowote tunaipelekea TFF kudai haki yetu kwa mchezaji Bonny na Kocha Nsajigwa ambao walitutoroka wakati wakitambua bado wana mikataba na sisi,” alisema Changawa.



0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic