October 10, 2013


LEWIS ALIPOMVAA VITALI


Bondia mstaafu ambaye alikuwa hapigiki, Lennox Lewis huenda akarejea ulingoni na kupigana na mmoja wa ndugu wa wawili, yaani mmoja wa akina Klitschko.

Lewis mwenye miaka 48, listaafu akiwa hajapiga katika mabondia wa uzito wa juu na imeelezwa ameahidiwa kupewa dola milioni 100 (zaidi ya Sh bilioni 1.6) iwapo atakubali kurejea na kupigana na mmoja kati ya akina Klitschko.
 
VITALI ALIPIGANA MARA YA MWISHO ZAIDI YA MWAKA

Imeelezwa promota wa Kirusi amemshawishi Lewis raia wa Uingereza ambaye amekubali kurejea na ameseama anataka miezi sita kabla ya kupanda ulingoni.

Ingawa Vitali Klitschko ndiye anamtaka Lewis kwa kuwa alimpiga mwanzoni mwa miaka ya 2000 katika ushindi uliozua utata, taarifa zinasema Muingereza huyo huenda akapewa azichape na mdogo wake Wladimir Klitschko.


Wiki iliyopita Wladimir alimchapa Mrusi Alexander Povetkin na inaelezwa alipewa dola milioni 50 katika pambano hilo.

Iwapo atarejea na kupigana na kati ya ndugu hao wawili, huenda likawa pambano kubwa zaidi la kihistoria katika mchezo wa ngumi katika karne hii.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic