October 10, 2013



 
BAADHI YA WACHEZAJI WA YANGA BAADA YA KUTUA LEO MJINI BUKOBA
Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara, Yanga wamefanikiwa kutua salama mjini Bukoba kwa usafiri wa ndege.


Yanga ina kibarua cha kuivaa Kagera Sugar, keshokutwa katika mechi inayotajiwa kuwa kali.

Kocha Mkuu wa Yanga, Ernie Brandts amesema wametua salama na mambo yanakwenda vizuri.

“Safari kutoka Dar es Salaam, tulipita Mwanza na sasa tupo hapa Bukoba. Tutafanya mazoezi leo jioni pia asubuhi.

“Hali ya hewa kidogo ni baridi, hivyo lazima tufanye mazoezi zaidi ya mara moja,” alisema.

Kagera Sugar ni kati ya timu zenye uwezo mkubwa na Yanga italazimika kufanya kazi ya ziada kwa kuwa mara nyingi imekuwa ikipata wakati mgumu katika uwanja wa Kaitaba mjini humo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic