October 11, 2013



 
TWITTE NA STAILI YA ZAMANI
Beki kiraka wa Yanga SC, Mbuyu Twite amekuja na staili mpya ya nywele na kuahidi kutoibadilisha mpaka mwisho wa msimu huu wa ligi kwa madai ya kuheshimu maamuzi ya mkewe juu ya nywele hizo.


Twite alionekana kwa mara ya kwanza akiwa na staili hiyo alipokuwa kwenye mazoezi ya timu hiyo yanayofanyika kwenye Uwanja wa Shule ya Sekondari ya Loyola iliyopo Mabibo jijini Dar es Salaam.

Nywele za beki huyo raia wa Rwanda zilikuwa zimesukwa kati kati ya kichwa pekee huku nyingine za pembeni za upande wa kushoto na kulia za kichwa chake zikiwa zimekatwa na kubaki ndogo kiasi cha kutoonekana kabisa mtu anapokuwa mbali.

Akizungumza na Championi Ijumaa juu ya staili yake hiyo mpya alisema kuwa alitaka kubadilisha staili ya nywele na ndipo alipokaa na mkewe kushauriana kuwa amsuke staili ipi ambayo ni nzuri na ndipo walipoptana asukwe hiyo.

“Alinisuka mke wangu, yeye pia alitoa ushauri juu ya staili mpya niliyotaka kusuka ndiyo akanisuka kama hivi na kwa ajili ya heshima yake juu ya nywele hizi sitozibadilisha mpaka msimu huu wa ligi uishe,” alisema Twite beki wa APR ya Rwanda.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic