Mashabiki
wa Napoli, wamewadunda wa Arsenal ikiwa ni sehemu ya kulipa kisasi baada ya
timu yao kuchapwa mabao 2-0.
Katika
vurugu hizo, shabiki mmoja wa Arsenal alijeruhiwa na kukimbizwa hospitali baada
ya kuwa amechanika usoni.
Mara
baada ya mechi hiyo ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, mashabiki wa Napoli walitoka
kweye Uwanja wa Emirates wakiwa na hasira na kuanza kuwashambulia wale wa
Arsenall.
Walikwenda
moja kwa moja katika eneo la Piebury Corner ambalo ni maarufu kwa mashabiki wa
Arsenal kila kunapokuwa na mechi kwenye Uwanja wao wa nyumbani wa Emirates na
kuanza kuwashambulia.
Walivunja
vioo kwenye mgahawa huo huku wakitumia mawe na viti na baadhi walikuwa na
mikanda waliyoitumia kuwachapa wengine.
Napoli
ni kati ya mji unaoongoza kwa kuwa na vijana wababe nchini Italia, timu nyingi
zimekuwa na hofu kubwa hasa mashabiki wao zinapokwenda kucheza kwenye mji huo.
0 COMMENTS:
Post a Comment