October 4, 2013



Mwenyekiti wa Mbeya City, Mussa Mapunda amesema wakati wa kukimbizana na ubingwa wa Ligi Kuu Bara umewadia, kauli hiyo imekuja ikiwa ni siku chache baada ya timu hiyo kuzikomalia Simba na Yanga katika mechi zao.


Mapunda amesema timu yao kwa sasa ina kila sababu ya kuwania ubingwa kwani wamemaliza kazi ngumu katika mzunguko wa kwanza kwa kucheza dhidi ya hii ya Yanga, Azam FC, Simba, Kagera na Mtibwa ambazo huaminika kuwa timu kubwa kwenye ligi hiyo.

“Nahisi ni muda muafaka kuwa kuwania ubingwa baada ya mechi ngumu za vigogo wa ligi. Kocha na wachezaji wote mpaka sasa hawaamini matokeo timu yetu iliyoyapata ukilinganisha na uzoefu wetu kwenye ligi.

“Naamini tunao uwezo wa kushinda kwa timu ndogo zilizobaki,” alisema Mapunda ambaye timu yake itaivaa JKT Oljoro, kesho Jumamosi kwenye Uwanja wa Sheik Amri Abeid, Arusha.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic