Na Saleh Ally
Kiungo wa Yanga, Haruna Niyonzima amepata
msiba mkubwa baada ya mwanaye kuanguka na kufariki dunia wakati akicheza na
wenzake.
Mtoto huyo wa Niyonzima, Akbar aliyekuwa na
umri wa miaka miwili na nusu, alianguka ghafla na kufariki dunia wakati
akicheza na wenzake jijini Kampala, Uganda, mwanzoni mwa wiki hii.
“Mtoto wa Haruna ameanguka na kufariki dunia
kule Uganda,” mtoa habari kutoka Kigali, Rwanda alilipasha Championi Ijumaa.
Blogu hii ilifuatilia ili kupata
uhakika kuhusiana na tukio hilo na lilifika nyumbani kwake jijini Dar es Salaam
na kumkuta mwanaye na mkewe.
Niyonzima raia wa Rwanda, alionekana
kutopenda kulizungumzia kwa undani suala hilo.
“Ni kweli nimepata msiba wa mwanangu lakini
nimekuwa na matatizo mengi yananiandama hadi nachanganyikiwa kwa kweli.
Ningependa mniache kidogo,” alisema kiungo huyo kwa sauti ya taratibu.
Kweli Niyonzima, amendamwa na majanga kwa
kuwa jana aliunguliwa na nyumba aliyokuwa akiishi katika eneo la Magomeni
Makuti jijini Dar.
Hivyo, Blogu hii ikaendelea kufanya
uchunguzi zaidi na kugundua mtoto huyo wa Niyonzima alikuwa akiishi na mama
yake nchini Uganda.
“Tayari Haruna amempa nauli mdogo wake
akashughulikie masuala ya msiba, yeye alikuwa na majukumu mengine lakini pia
kama unavyoona, nyumba yake imeungua,” kilieleza chanzo kingine.
“Yule mtoto awali alikuwa Kigali lakini
baadaye akahamia Kampala baada ya mama yake kupata kazi huko Uganda na walikuwa
wakiishi huko.”
Niyonzima anaishi Magomeni Makuti jijini Dar
pamoja mkewe na mwanaye Ramzey mwenye miaka takribani mitano.
Awali kulikuwa na taarifa za kuchanganya
baada ya kusikika kuwa amepata msiba wa mwanaye, lakini ukweli si yule anayeishi
naye nini Dar ambaye anajulikana kwa rafiki zake na mashabiki wengi wa soka
nchini.
Stori ya ukurasa wa pili katika gazeti hili
inaeleza vizuri zaidi kuhusiana na mkasa wa kuunguliwa nyumba yake. Isome.
Nadir Haroub ‘Cannavaro’ na Kelvin Yondani
kwenye mechi za Ligi Kuu Tanzania Bara.
SOURCE: CHAMPIONI
Pole sana Niyonzima-ni mapito tuu hayo
ReplyDelete