Pambano la Ligi Kuu ya Vodacom kati ya Simba na Azam
lililochezwa jana (Oktoba 28 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam
limeingiza sh. 64,261,000.
Washabiki waliohudhuria mechi hiyo namba 76
iliyomalizika kwa Azam kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 walikuwa 10,728 ambapo
viingilio vilikuwa sh. 5,000, sh. 8,000, sh. 15,000 na sh. 20,000.
Mgawo wa mapato hayo ulikuwa kama ifuatavyo; Kodi ya
Ongezeko la Thamani (VAT) sh. 9,802,525.42, gharama za kuchapa tiketi sh.
3,793,490 wakati kila klabu ilipata sh. 14,946,170.45.
Wamiliki wa uwanja walipata sh.
7,599,747.49, gharama za mchezo sh. 4,599,848.61, Bodi ya Ligi sh.
4,599,848.61, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 2,279,924.31,
Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 1,773,274.46.
0 COMMENTS:
Post a Comment