October 10, 2013




Kikosi cha Simba kiko katika nafasi nzuri ya kucheza mpira wa ushindani katika mechi yao ya keshokutwa dhidi ya Prisons ya Mbeya.

Simba inaikaribisha timu ngumu ya Prisons keshokutwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar.

Kocha Mkuu, Abdallah King Kibadeni amesema watakachofanya ni kuangalia siku ya kesho.

“Hadi sasa tuko vizuri, vijana wana morali tofauti na mambo mengi yanayozungumzwa na mategemeo yetu ni kufanya vizuri,” alisema.

Simba inaongoza ligi hiyo kwa kuwa na pointi 15 ikifuatiwa kwa karibu na Azam FC ambayo jana iliitungua Mgambo Shooting kwa mabao 2-0.
“Prisons ni timu imara, lazima tujitume na tunatambua umuhimu wa hilo. Tumezungumza na vijana na tutazungumza nao tena kwa kuwa pointi tatu ni muhimu sana,” alisema Kibadeni.
Bado Simba haijafunguka vizuri na kuonyesha soka la kuvutia katika mechi zake zilizopita.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic