Mshambuliaji wa Simba, Amissi Tambwe
amesema kuwa hana mpango wa kuwaangalia na hawaogopi mabeki wa Yanga, Nadir
Haroub ‘Cannavaro’ na Kelvin Yondani kwenye mechi za Ligi Kuu Tanzania Bara.
Mrundi huyo ambaye ameanza kwa kasi ya
kufunga mabao saba kwenye mechi tano alizocheza, ameonekana tishio kwa timu
shiriki za ligi hiyo.
Akizungumza na Championi Ijumaa, Tambwe
alisema hana mpango wa kwenda uwanjani kwa ajili ya kuwaangalia Yondani na
Cannavaro wakicheza mechi za ligi hiyo kabla ya kuvaana nao Oktoba 20, siku
anayoamini lazima watakutana kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
“Sina mpango wa kwenda uwanjani kabla
kucheza nao kwa ajili ya kuangalia uwezo na aina ya uchezaji ya mabeki wa
Yanga, nitaonana nao uwanjani siku ikifika.
“Nitaonana nao nikiwa uwanjani, wao
wananizuia na mimi nikitaka kufunga, lakini licha ya hayo yote ninaheshimu
uwezo wao, ninaamini ni wachezaji wazuri,” alisema Tambwe.
Huenda kukawa na ushindani mkali kati ya
Yondani na Tambwe kwa kuwa wote wana kasi na wepesi katika kuiwahi mipira
katika kuokoa au kufunga.
0 COMMENTS:
Post a Comment