Beki mahiri wa Ruvu Shooting, George Michael
amepewa jukumu la kuhakikisha mshambuliaji wa Simba, Amissi Tambwe hafurukuti katika
mechi ya Ligi Kuu Bara dhidi ya timu hiyo kwenye Uwanja wa Taifa, Dar.
Ofisa Habari wa Ruvu Shooting, Masau Bwire amesema
Michael alipewa jukumu hilo na kocha wake, Charles Mkwasa kuhakikisha Tambwe
hapati nafasi kama alivyoweza kumdhibiti nyota wa kimataifa wa Yanga, Didier
Kavumbagu na winga Simon Msuva katika dhidi ya Yanga, wiki iliyopita.
Licha ya kufungwa na Yanga bao 1-0, lakini
beki huyo alikuwa gumzo kwa mashabiki kutokana na kiwango kizuri alichoonyesha.
“Kwani Tambwe ndiyo nani? Kama Yanga walinyoosha
mikono kwa nini asiwe yeye. Mpango wa kocha si kumtazama Tambwe tu, sema
tumejiwekea utaratibu wachezaji wote kujua majukumu yao uwanjani.
“Tunajaribu kuwatengeneza kina Michael wengi
kabla ya mchezo wa kesho. Siku zote Ruvu Shooting haigopi jina wala kiwango cha
mtu na kila mchezaji ameishapewa jukumu lake kuelekea mchezo huo,” alitamba
Bwire.
Tambwe ambaye ni raia wa Burundi pia
mfungaji bora wa michuano ya Cecafa 2013, ndiye kinara wa mabao mpaka sasa katika ligi kuu akiwa na mabao saba.
0 COMMENTS:
Post a Comment