November 1, 2013


Katika hali isiyo ya kawaida, Uwanja wa Mabatini unaotumiwa na Ruvu Shooting kama uwanja wa nyumbani, umetawaliwa na wavuta bangi.


Katika mechi ya Ruvu dhidi ya Kagera Sugar lilishuhudia vijana kadhaa waliojitenga kwenye sehemumoja ya jukwaa uwanjani hapo, wakivuta kilevi hicho wakati mechi ikiendelea.

Kama hiyo haitoshi, baada ya muda walianza kutoa lugha kali kuelekea kwa wachezaji wa Kagera Sugar kila walipokuwa wakigusa mpira.

Aidha, tukio la kushangaza lililootokea uwanjani hapo ni gazeti hili kushuhudia wachezaji wakiogea katika chumba kisicho na mlango huku wengine wakijisitili kwa kujipanza kwenye kuta za jukwaa la mashabiki kushoto mwa jukwaa kuu, sehemu ambayo haijengwa vema.


Suala la matatizo ya viwanja vibovu katika Ligi Kuu Tanzania Bara ni tatizo sugu lakini wamiliki na waangalizi wa viwanja hivyo wamekuwa wagumu kutoa ufafanuzi na kufanyia marekebisho.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic