November 1, 2013


Kiungo Salum Telela wa Yanga, anatarajiwa kurejea dimbani kuendelea kuitumikia timu yake hiyo Januari, mwakani katika mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Bara.


Telela aliumia enka ya mguu wa kulia kwenye mechi dhidi ya Tanzania Prisons ambapo ilimlazimu kukaa nje ya uwanja kwa muda wa mwezi mzima ambapo baada ya kupona anahitaji mazoezi mepesi kwa ajili ya kukaa sawa ili apone kabisa. 

Telela amesema amepona kabisa, lakini amepewa muda wa kujiweka sawa zaidi kwa ajili ya kurudi vema msimu ujao kwa sababu muda aliopewa na mechi zilizobaki ni chache.

“Nimepewa muda wa kupumzika kwa ajili ya kujiweka vema ili nikirudi nianze upya, kwa hiyo sitakuwepo mpaka mzunguko huu unamalizika.  Nitakuwepo kwenye mzunguko wa pili Januari,” alisema Telela.


Zimebaki mechi mbili kwa kila timu kumaliza mechi zake za mzunguko wa kwanza ambapo mzunguko wa pili unatarajiwa kuanza Januari 25 mwakani, kwa Yanga kuivaa Ashanti, mechi itakayopigwa Uwanja wa Taifa jijini Dar. 

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic