November 24, 2013


Mabingwa wa Ulaya, Bayern Munich wameonyesha wamepania kuendelea kuwa mabingwa wa Ulaya baada ya ushindi safi wa mabao 3-0 dhidi ya wapinzani wao wakubwa Borussia Dortmund.


Bila ya kujali Dortmund wanaovaa njano na nyeusi wako nyumbani, Bayern wamewatungua bao hizo huku wakiwaonyesha soka safi.

Mabao ya Bayern yalifungwa na Mario Gotze katika dakika ya 66, kumbuka nyota huyu amejiunga na Bayern akitokea Dortmund, msimu huu.

Baadaye Arjen Robben akaongeza msumari wa pili katika dakika ya 85, huku ikionekana Dortmund ikutafuta bao la kufutia machozi, Bayern ikaongeza la tatu katika dakika ya 87, Thomas Muller akiingia kimiani.


Pamoja na kuwa ugenini, Bayern walitawala mchezo huo kwa muda wote wakianzia kipindi cha kwanza na wenyeji walikuwa wakifanya mashambulizi machache ambayo yalionyesha kuwa na nguvu lakini hayakuzaa matunda.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic