November 24, 2013


RAGE AKIZUNGUMZA LEO

Mwenyekiti aliyesimamishwa Simba, Ismail Aden Rage amekaidi agizo lililotolewa na TFF la kuitisha mkutano wa dharura wa wanachama ndani ya siku 14.

Pamoja na hivyo, Rage amesema kama TFF itaendelea kumshinikiza, basi mara moja atajiuzulu.

Rais wa TFF, Jamal Malinzi alimsisitiza Rage kufanya hivyo ili kulitatua tatizo lililojitokeza. Rage ameyasema hayo katika mkutano na waandishi wa habari uliomalizika punde katika makao makuu ya Simba jijini Dar.

Pia Malinzi akaahidi kutuma mjumbe wa TFF ambaye atakwenda kusimamia mkutano huo huku akisisitiza suala la haki lichukue nafasi.

1 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic