November 1, 2013



Katika hali isiyokuwa ya kawaida mashabiki wa Yanga walimzomea kipa namba moja wa timu hiyo Ally Mustafa ‘Barthez’ wakati akionyeshwa kupitia runinga iliyokuwa ikirusha matangazo kwenye Uwanja wa Taifa, Jumanne wiki hii.


Barthez alionyeshwa wakati anapasha kwa ajili ya kujiweka fiti ili kwenda kuchukua nafasi ya kipa Deogratius Munishi ‘Dida’ aliyeumia kwenye mechi dhidi ya Mgambo Shootings, ndipo kamera zilipommulika na mashabiki kuanza kumzomea.

Hata hivyo kipa huyo aliendelea kupasha na kupuuzia kelele hizo za mashabiki wa Yanga, ambao wanalalamikia wakidai uwezo wake umeshuka kutokana na kushindwa kuzuia mabao yaliyofungwa katika mchezo dhidi ya Simba, wiki mbili zilizopita na kutoka sare ya 3-3.

Lakini hata hivyo Barthez hakuingia kucheza mechi hiyo kutokana na Dida kutibiwa na kuendelea na mchezo ambao walifanikiwa kushinda kwa mabao 3-0.

Alipoulizwa Razak Siwa ambaye ni kocha wa makipa wa timu hiyo, alisema: “Mimi siwaangalii mashabiki, kikubwa yeye mwenyewe aendelee kufanya mazoezi zaidi na kuachana na kelele hizo mashabiki. Hali hiyo ni ya kawaida kwa mchezaji yeyote.”  


Aidha, Kocha Mkuu wa Yanga, Ernie Brandts alisema alichukizwa na tukio hilo. “Sikupenda tabia ile iliyoonyeshwa na mashabiki, hawakumfanyia kitu kizuri, nafikiri walitakiwa kumsaidia kwa kumpa moyo au hata kumshauri kama wakipata nafasi siyo kumzomea,” alisema Brandts. 

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic