November 1, 2013

KIBADENI, JULIO (KUSHOTO) WAKIWA NA NICO NYAGAWA NA JAMES KISAKA KATIKA BENCHI LA SIMBA

Katika hali isiyokuwa ya kawaida inaelezwa kuwa wachezaji wa Simba wamewatengenezea ujumbe mfupi wa maneno makocha wao, Abdallah Kibadeni na msaidizi wake, Jamhuri Kiwhelo ‘Julio’ wakiwataka na wao warudi kukinoa kikosi cha Simba B.


SALEHJEMBE ilifanikiwa kupata ujumbe huo uliotumwa na rafiki wa mmoja wa wachezaji waliosimamishwa wakitaka na wao washushwe hadi timu B kutokana na kuchapwa na Azam 2-1 hali iliyosababisha kushika nafasi ya nne kabla ya mechi ya jana dhidi ya Kagera Sugar.

Ujumbe huo unasomeka hivi: “Kibadeni na Julio wamerudishwa timu B, Matola (Selemani) kapanda maana makubaliano ni kuongoza ligi katika raundi hii ya kwanza sasa wanashika nafasi ya nne na bado mechi mbili tu.”


Baada ya muda wachezaji hao hutuma ujumbe mwingine ulioandikwa: “Hiyo ni chemsha bongo tu hawajashushwa ila nimeandika hivyo maana wao mchezaji akicheza vibaya siku moja wanampeleka timu B, wao timu ipo nafasi ya nne sasa, basi nao waende timu B ili wajue kuwa mpira ni mchezo wa makosa waache kutoa shutuma kwa wachezaji bhana.”

SOURCE: CHAMPIONI

2 COMMENTS:

  1. kiukweli mie siwakubali makocha wa samba, wameua vipaji walivyo vikuta,..kocha mpaka leo huna first eleven wanatia aibu na rage wao,...unamuondoa kocha mwenye vyeti vya UEFA mnatuletea mwenye vyeti vya FAT

    ReplyDelete
    Replies
    1. hata mie naunga mkono waondolewe ,unaweza vipi kumpeleka chanongo tim B au henry makocha wamejaa majungu na uswahili..Milovan alitukanwa matusi ya nguoni na mafisango(RIP) akamsamehe akamrudisha kundini leo kibaden analeta mambo ya Kiswahili tu,

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic