November 1, 2013


Beki wa Yanga, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ amesema sababu kubwa ya kutemwa kwake kwenye kikosi cha Zanzibar Heroes siyo suala la kushuka kiwango ila ni kwa kuwa hakurudisha fedha walizogawana wachezaji wa timu hiyo mara baada ya kushika nafasi ya tatu katika Kombe la Chalenji, mwaka jana.


Cannavaro ni mmoja wa wachezaji waliotemwa katika kikosi hicho kinachojiandaa kwa ajili ya michuano hiyo tena ambayo inatrajiwa kuanza Novemba 27, mwaka huu nchini Kenya.

“Kocha (Salum) Bausi ameacha kuniita siyo kwa sababu ya kiwango ila ni kile kisa cha kutorudisha fedha tulizojigawia za mshindi wa tatu katika michuano iliyopita,” alisema Cannacaro.

Wachezaji wa Zanzibar Heroes waligawana fedha hizo kwa kile walichodai zingefika kwa viongozi wala wasingezipata.


“Mbona timu ya taifa nipo na Yanga napata namba kama kawaida na mimi ndiyo nahodha. Mimi nimeridhika kutoitwa, kwa sababu timu ina wachezaji wengi wazuri. Naitakia kila la kheri timu yangu na wala sina kinyongo nayo,” alisema.

SOURCE: CHAMOPIONI

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic