November 1, 2013


Kocha Mkuu wa Azam FC, Stewart Hall amefunguka kuwa atamuweka nje mshambuliaji wake mkongwe, Gaudence Mwaikimba kwenye kikosi chake kwa kuwa mchezaji huyo amechoka baada ya kumtumia kwenye mechi nyingi.


Inaelezwa kuwa Mwaikimba ameanza mapumziko hayo kwenye mechi ya Ligi Kuu Tanzania Bara ya timu yake dhidi ya Simba, Jumatatu ya wiki hii.

Stewart alisema kuna uwezekano wa Mwaikimba kuwa nje katika mechi mbili zijazo za kukamilisha mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Ruvu Shooting na Mbeya City.


“Mwaikimba hana majeraha yoyote, nimeamua kumpumzisha katika mechi hizi tatu, kuanzia ile ya Simba na hizi mbili zilizobaki za kumalizia mzunguko wa kwanza wa ligi, sababu ni kuwa ametumika kwenye mechi nyingi,” alisema Stewart.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic