November 20, 2013





Imeelezwa kuwa dau la usajili la kipa namba moja wa Mtibwa Sugar, Hussein Sharifu ‘Casillas’, ndilo limesababisha ashindwe kutua kuichezea Simba inayomwania.


Kipa huyo ameingia kwenye orodha ya makipa wanaowaniwa vikali na timu hiyo, akiwemo Ivo Mapunda anayeichezea Gor Mahia ya Kenya.

Akizungumza na Championi Jumatano, Casillas alisema kuwa yeye hana tatizo kwani Simba walishamfuata na tayari ameshawatajia dau lake, kilichobaki wao wenyewe wakamilishe kiasi hicho cha fedha yeye avae jezi nyekundu.

Casillas alisema yeye hana haraka, anawasubiri mara watakapokubaliana katika kutoa dau hilo ambalo ni siri, akaongeza kwamba mara moja atasaini mkataba wa kuichezea timu hiyo katika dirisha dogo.

“Meneja wangu tayari amewatajia Simba dau la usajili tunalolitaka, hivyo tunawasubiri watakapokuwa tayari watoe haraka fedha hiyo nami nitasaini mkataba husika.

“Mimi ninachoangalia ni maslahi pekee, siyo kingine na sina haraka, wenyewe wamalizane na meneja wangu tu, kama wakishindwa nitaendelea kuichezea timu yangu ya Mtibwa Sugar,” alisema Casillas ambaye aliitwa kwenye kikosi cha kwanza cha timu ya taifa kabla hajatemwa.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic