November 20, 2013

CHACHA ALIPOKUWA YANGA



Beki wa zamani wa Yanga, Chacha Marwa, Jumamosi ya wiki iliyopita alizichapa na mshambuliaji wa zamani wa Simba, Ally Ahmed Shiboli, kwenye mechi ya kuwania Kombe la Ng’ombe iliyopigwa katika Uwanja wa Sinai, Vingunguti jijini Dar.


Chanzo cha karibu na wachezaji hao kilisema Chacha alikuwa akiichezea Faru Jeuri na Shiboli akiwa na Soweto.
 
SHIBOLI ALIPOKUWA SIMBA

Chacha wakati akigombea mpira alipigwa kichwa na Shiboli hadi akamchana mdomo, hali iliyomkasirisha beki huyo wa kati na kuamua kwenda kumrushia ngumi Shiboli na ndipo vurugu zilipoanza. 

Alisema hata hivyo, Shiboli naye alikuja juu na vita ikaanza lakini mashabiki na viongozi wa timu hizo waliwahi na kuwaamua.

Hata hivyo, baada ya kuwaamua, mashabiki walimvamia mwamuzi wa mchezo huo ambaye ni mchezaji wa zamani wa Yanga na Simba, Ephraim Makoye, kwa madai kuwa anapendelea.

Baada ya vurugu hizo, Makoye alitoka nduki na filimbi yake mkononi hali iliyosababisha mchezo huo kuvunjika.

 “Mechi haikuisha kutokana na vurugu iliyoanzia kwa wachezaji Chacha na Shiboli ambao walipigana uwanjani, hivyo mpira ukasimama kwa ajili ya kuwaamua lakini tukashangaa na refa naye wanampiga wakati hakuwa na kosa lolote.  

 Ikabidi akimbie na mpira ukawa umeishia hapohapo dakika ya 77 huku kina Shiboli wakiongoza kwa bao 1-0,” kilisema chanzo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic