November 20, 2013



 
JUMA (KULIA) AKIWA NA JUMA ABDUL WA YANGA
Timu ya Mtibwa Sugar imebariki aliyekuwa kiungo wao, Awadhi Juma, kutua katika kikosi cha Simba.


Awadhi ambaye aliichezea Mtibwa Sugar kabla ya kutua Thailand katika klabu ya Criracha FC, inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza, ametua Simba kwa mkataba wa miaka miwili.

Mratibu wa Mtibwa Sugar, Jamal Bayser, alisema hawana shida na mchezaji huyo kutua Simba kwani atawasaidia katika mzunguko wa pili, pia kwa upande wao walishamalizana naye na ni mchezaji huru.

“Awadhi ni mchezaji mzuri na hakuna shida kutua Simba kwa kuwa ni mchezaji huru, alishamaliza mkataba na sisi, hivyo atawasaidia sana Simba kwani ni mchezaji mzuri.

“Sisi kama Mtibwa tunatarajia kukutana ndani ya wiki hii kujadili ripoti ya kocha Mecky Maxime kwa ajili ya kuanza mchakato wa usajili wa wachezaji wapya,” alisema Jamal.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic