November 12, 2013


Kiungo nyota wa Barcelona, Cesc Fabregas amesema mshambuliaji wa timu hiyo, Lionel Messi anahitaji kupumzika.


Fabregas amesema Messi amecheza mechi nyingi sana kwa kujituma hali ambayo imekuwa ikisababisha aumie karibu kila mara.
“Anahitaji kupumzika hata kidogo kabla ya kurejea akiwa katika hali nzuri, amechoka na utaona siku zote ni mchezaji wmenye juhudi kubwa uwanjani na wengi wanataka kumzuia.

“Hali kama hiyo iliwahi kunitokea wakati nikiwa Arsenal, kwa kiasi kikubwa inachanganya na hasa usipotulia,” alisema.
Hivi karibuni Messi amekuwa akiumia mfululizo, hali inayosababisha aendelee kuwa gumzo kama kweli atafanya vziuri katika misimu inayokuja.

Tayari Kocha Mkuu wa Argentina, Alejandro Sabella ameishatangaza kwamba kutokana na hali yake sasa, huenda akamuacha Messi katika kikosi chake wiki hii kwa ajili ya mechi ya kirafiki.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic