November 13, 2013


Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Kim Poulsen amesema kipigo cha bao 1-0 walichokipata kikosi hicho ni changamoto.


Stars imelala kwa bao 1-0 dhidi ya Future Taifa Stars katika mchezo wa kirafiki uliochezwa leo kwenye Karume jijini Dar.

Akizungumza jioni hii, Poulsen alisema ushindani wa timu hizo mbili ulionyesha kuna kitu na waliofungwa wanapaswa kujiuliza.

“Ilikuwa mechi nzuri na utaona namna upinzani ulivyokuwa, lakini ni sehemu ya changamoto kwa walio katika kikosi cha Taifa Stars,” alisema.

“Tuna mechi ngumu dhidi ya Kenya, hivyo lazima tuwe tayari kabla ya kucheza nao kwa kuwa tutakuwa nyumbani,” alisema.

Taifa Stars itawavaa Harambee Stars Jumanne ijayo kwenye Uwanja wa Taifa katika mechi ya kirafiki inayosubiriwa kwa hamu na mashabiki.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic