November 14, 2013


Beki wa zamani wa Arsenal, William Gallas amefanya mazoezi pamoja na beki Mtanzania Shomari Kapombe.

Kapombe na Gallas wamefanya mazoezi kwenye kikosi cha daraja la nne nchini Ufaransa cha AS Cannes anachokichezea Mtanzania huyo.



Katika mazoezi hayo, Kapombe alikuwa kikosi kimoja na Gallas ambaye aliwahi kung’ara Ligi Kuu England pia akiwa na Spurs.



Mtanzania huyo aliyekuwa ameumia, tayari amerejea kazini na alianza katika mechi ambayo timu yake ilitoka sare ya bao 1-1 wiki iliyopita.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic