November 13, 2013

TAMBWE
Uongozi wa Simba umeamua kukata mzizi wa fitna kuhusiana na suala la wachezaji wake Amiss Tambwe na Haruna Chanongo na kusema hawauzwi.


Kuwepo kwa taarifa kwamba wako sokoni na Yanga imekuwa ikinyata, kumeifanya Simba kufunguka.

Mwenyekiti wa Simba, Ismail Aden Rage amesema wachezaji hao hawauzwi.

“Hawauzwi na kama kuna mtu anafikiri hivyo basi anajisumbua,” alisema.

“Kweli Simba tuna sera ya kuuza wachezaji lakini kwa hawa hatuhitaji na badala yake tunaboresha kikosi ili tupambane kwenye ligi.”

Tambwe ndiye tegemeo katika ufungaji Simba, anaongoza wapachika mabao wa Ligi Kuu Bara, lakini Chanongo ni kati ya wachezaji wanaochipukia kwa kasi katika soka nchini na amekuwa msaada mkubwa.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic