November 13, 2013

IVO (ALIYEANGUKA) AKIWA MAZOEZINI NA GOR MAHIA KWENYE UWANJA WA CITY JIJINI NAIROBI, JUMAMOSI ILIYOPITA

Kipa wa Gor Mahia, Ivo Mapunda leo ameichezea tena Taifa Stars baada ya kuachwa kwa zaidi ya miaka mitatu.

Katika mechi mazoezi dhidi ya Future Taifa Stars, Ivo aliingia kipindi cha pili kuchukua nafasi ya Ally Mustapha ‘Barthez’ aliyekuwa tayari kafungwa bao 1-0 la Elias Maguri.

Ivo alifanikiwa kudaka kwa dakika zote 45 bila ya nyavu zake kutikiswa.

Awali, Poulsen aliamua kumtema Ivo lakini baadaye iligundulika TFF haikuwa imefikisha barua katika Shirikisho la Soka la Kenya (FKF) ambalo lingepeleka kwa timu yake.


Ivo aliamua kuzungumza na TFF ambao walimueleza kuhusiana na kuachwa kwake, lakini baadaye inaelezwa alizungumza na Poulsen ambaye baadaye aligundua kipa huyo hakuwa na tatizo na kumrudisha.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic