November 13, 2013


Rais wa TFF, Jamal Malinzi leo aliibuka katika mechi mazoezi kati ya vikosi vya Taifa Stars dhidi ya Future Taifa Stars kwenye Uwanja wa Karume jijini Dar.


Baada ya kushuhudia mechi hiyo kwa dakika 45, Malinzi alizungumza na wachezaji hao na kuwasisitiza Stars kwamba waitandike Kenya.

Stars itaivaa Harambee Stars katika mechi ya kirafiki itakayopigwa Jumanne kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar.
Pamoja na kuwataka washinde, Malinzi aliwasisitiza wachezaji hao hasa kwa watakaopata nafasi ya kwenda nchini Kenya katika michuano ya Chalenji, kuhakikisha wanafanya vema.

“Lakini bado nasisitiza suala la nidhamu, sipendi mkirudi hapa tuanze kutafutana katika suala la adhabu,” alisema Malinzi.


Hii ni mara yake ya kwanza kufika mazoezini Taifa Stars akionyesha utendaji kwa vitendo zaidi badala ya maneno tu.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic