November 23, 2013



Rais wa TFF, Jamal Malinzi amempa siku 14 mwenyekiti wa Simba aliyesimamishwa kuitisha mkutano mkuu wa dharura wa wanachama.

Malinzi amemtaka Rage kufanya hivyo mara moja ili kulipatia usumbufu tatizo la kusimamishwa kwake kwa kuwa TFF imepata barua kutoka sehemu mbili.

“Tumepokea barua kutoka kwa kamati ya utendaji ya Simba iliyomsimamisha Rage ikielezea kuhusiana na kusimamishwa kwake, lakini pia Rage ametupa barua akisema hatambui lolote kuhusiana na hilo.

“Hivyo nimempa ndani ya siku 14 awe amefanya hivyo ili ufumbuzi wa suala hili upatikane,” alisema Malinzi.

Tayari kamati ya utendaji ya Simba ilikuwa imeitisha mkutano huo wa wanachama Desemba Mosi ambayo ni ndani ya siku hizo 14.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic