November 22, 2013



 
MBEYA CITY U20
Michuano ya Uhai Cup inayoshirikisha timu za vikosi vya vijana walio na umri chini ya miaka 20 imeendelea jana na juzi kwenye viwanja mbalimbali huku timu kama za Mbeya City, Azam FC na Kagera Sugar zikifanya vizuri.


Katika mechi iliyopigwa jana kwenye Uwanja wa Karume uliopo Ilala jijini Dar, timu ya JKT Oljoro ilifanikiwa kuichapa Ruvu Shooting kwa bao 1-0.

Aidha, katika mchezo mwingine uliopigwa juzi kwenye Uwanja wa Chamazi, Dar timu ya Azam iliifunga Yanga mabao 2-0, wafungaji wakiwa ni Adam Omari dakika ya saba na Gadiel Michael dakika ya 39.

Mbeya City waliichakaza JKT Ruvu ya Pwani kwa bao 1-0, lililotupiwa nyavuni na Gerrard Mbena dakika ya 80 kwenye Uwanja wa Chuo cha DUCE, Temeke jijini Dar.

Katika michezo mingine iliyopigwa Karume juzi kwa nyakati tofauti, Rhino Rangers ya Tabora iliibutua Mtibwa ya Morogoro kwa bao 1-0 huku Kagera Sugar ya mkoani Kagera ikiikalisha Tanzania Prisons kwa mabao 2-0.  

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic